بسم الله الرحمن الرحيم


بسم الله الرحمن الرحيم

UDOMSA.

Saturday, 8 October 2011

TUWEKE MAZINGATIO

Bismillah.
Assalamu Alaiekum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Ilitokezea Siku Mmoja Katika Waja Wa Mwenyezi Mungu. Huyu Mja Alikuwa Ameghafilika Ulimwenguni. Siku Mmoja Alirejea Nyumbani Mchana Na Kula Chakula Cha Mjana Na Kwenda Kulala .

Ghafla Katika Usingi Wake Aliona Mke Wake Anakuja Kumuamsha Na Alipofika Tu Akawa Anamuamsha Mume Wangu Amka Magharibi Imekaribia. Na Yule Mke Akaona Bwana Haamki Ikiwa Anamtikisa Kila Upande Bado Haamki. Na Yule Mume Anaona Kila Kitu Atachofanyiwa Mke Wake Na Alikuwa Anamjibu Mimi Nimeshaamka Usinitikise Mimi Niko Macho Mbona Unanitikisa. Na Mke Bado Anamuona Mumewe Amelala Tu Ikawa Mke Anajaribu Kutikisa Kichwa Bado Haamki Mke Akaaza Kulia.

Na Yule Mume Anamwambia Usilie Mimi Nikomacho Mbona Unalia Mke Alipoona Mumewe Yupo Katika Hali Ilie Alikwenda Kuwaita Kaka Zake Na Dada Zake Walipofika Na Wawoo Walijaribu Kumwita Wapi Kimwa. Na Wakati Huwo Yeye Anawaambia Mimi Nimeshaamka Vipi Nyinyi Munaanza Kulia Musilie Mimi Nimzima. Na Wale Kaka Na Dada Wakaamuwa Kumwita Daktari Ili Aje Kumtizama Vipi Mambo Haya.
Na Yule Mume Anasema Huku Amehamaki Na Wawoo Vipi Nyinyi Munalia Na Sasa munataka Kumwita Daktari Mimi Mzima Hapa Lakini Nyinyi Muna Akili Au Vipi. Daktari Alifika Na Kumtizama Yule Mume Na Alisema Huyu Ameshakufa Tena Kwa Muda Sasa. Na Yeye Anasema Aee Nyinyi Mimi Ni Mzima Vipi Nyinyi Muna Akili Lakini.

Wakafika Watu Wapale Mtaani Na Mshekhe Wakaanza Kumvua Nguwo Iliwakamuoshe. Walipoanza Tu Kumgusa Na Yeye Anasema Vipi Nyinyi Nyote Akili Zenu Ziko Sawa Mimi Ni Mzima Munanivuwa Nguwo Zangu Vipi Nyinyi Munanichukuwa Nakuniosha Kama Maiti Mimi Mzima Niwacheni Niwacheni Niwacheni. Watu Waliendelea Kumuosha Na Kuvisha Sanda Na Kumtia Katika Jeneza Na Yeye Anapinga Kelele Tu Huku. Na Walimpeleka Kumsalia Na Kumchukuwa Mpaka Kaburini. Bado Yeye Anasema Musinitie Kaburini Mimi Ni Mzima.

Na Watu Walimtia Kaburini Na Kufukia Na Yeye Anawaona Kila Mmoja Waoo Anasema Nyinyi Vipi Munanifukia Na Mimi Niko Haii.Na Watu Wakafukia Kaburi Na Kumuombea Duaa Na Kuondoka Kaburini.

Sasa Yeye Anaona Kiza Tuu Kwenye Kaburi Haoni Kitu Chochote Ghafla Anaona Watu Wa Wili Moja Kasimama Katika Kichwa Chake Na Moja Miguuni Mwake. Na Yule Aliesimama Katika Miguu Yake Akawa Anamuuliza Nani Mungu Wako Wewe. Na Yeye Ikawa Anajaribu Kujibu Lakini Anashindwa Kujibu Kujibu Kila Akijaribu Anashindwa Na Huku Anaulizwa. Sasa Yule Aliye Simama Kichwani Kwake Akamuuliza Suala La Pili Nani Mtume Wako Akawa Anajaribu Kujibu Ikawa Anashindwa Alimpinga Zaruba Mmoja Tu Na Kwa Ghafla Alizinduka Katika Usingizi Wake.

Kijasho Kinamtoka Alisema Mambo Makubwa Alikwenda Kutia Uzu Na Kuanza Kusali Na Kuomba Msamaha Kwa Makosa Yake Yote. Tokea Siku Hiio Yeye Sasa Ni Mtu Wa Dini Sana Mwenye Kushikamana Nyendo Zote Alizoamrishwa Na Mwenyezi Mungu Na Mtume Wake Muhammad S.A.W.

Waislamu Jee Sisi Vipi Hapa.

Shukran

Wenu Mwenye Kukutakieni Maisha Ya Salama Katika Dunia Na Akhera.

Friday, 29 July 2011

USHAURI WA BURE: LEO NA KESHO.

USHAURI WA BURE: LEO NA KESHO.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya: …………
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuisoma dini yako.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuisoma Quran na Maana yake.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kutafuta sadaka ya kujitolea kwa ajili ya uislamu iwe muda, hali na mali.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya familia yako kuzungumza nayo mambo ya dini.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kutembelea ndugu jamaa na marafiki.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya mkeo kama umeoa na mumeo kama umeolewa.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kumfikiria Allah (sw) na maneno yake na makatazo yake,
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuzifikiria neema na rehma alizokuneemesha mola wako.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kujiombea dua na usitegemee dua za misikitini na mikusanyiko.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuiendea riziki ya Allah aliokupangia na ukinai na kuridhika nayo.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuongeza ujuzi juu ya Elimu yako ya mazingira na jamii ikuzungukayo .
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuipata na kuitafuta elimu juu ya mwili wako na maumbile yako, kuepuka maradhi na madhara juu yake.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kujishughulisha na hidma mbalimbali kwa ajili yako, uislamu na jamii yako kwa ujumla.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kupumzika baada ya uchovu wa shughuli, mizunguko na fikra nzito.
Usisahau kutenga muda wako kwa ajili ya kuwakumbusha watu wako na wakaribu wako juu ya haya.
Ushauri huu utaendelea inshaalah, na mnaalikwa katika muendelezo huu kwa ajili ya kuusiana.
MUHIMU KUZINGATIA HAYA KWANI UJUMBE USHAWAFIKIA
WABILLAH TAWFIQ.