MAKOSA YA MSINGI YALIYOMO NDANI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MTAZAMO WA UISLAMU
Utangulizi
Sifa zote njema anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na Rehema na Amani zimshukie Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) na Radhi za Mola ziwafikie Maswahaba zake wote Kiramu na kila mwenye kufuata nyayo zao mpaka siku ya Qiyaamah.
Kitabu ”MAKOSA YA MSINGI YALIYOMO NDANI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MTAZAMO WA UISLAMU” ni mkusanyiko wa Maudhui mbali mbali zilizotolewa na wahadhiri na wasemaji mbali mbali katika semina maalumu juu ya maudhui hiyo hapo juu iliyokusanya wanachuoni, wanasheria, walinganiaji na wasomi mbali mbali waliojikusanya katika Ukumbi wa Chuo cha Wasichana cha UMMU SALAMAH, mnamo tarehe 25 Swafar 1432 H sawa na 30 Januari 2011 M, lengo la semina hiyo lilikuwa ni kutafakari maneno ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwataka wananchi wa Tanzania wakiwemo wanadini kuchangia maoni katika mchakato mzima wa kutungwa upya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Semina hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti Shaykh ‘Alliy Adamu ‘Alliy kutoka Msumbiji ilitoa mapendekezo kwamba katika hatua ya awali iko haja ya kueneza yaliyopatikana katika semina hiyo kwa njia ya makongamano mengine katika kiwango cha wilaya, mikoa na Kitaifa, pia kwa njia ya mihadhara mbali mbali, khutba za ijumaa na kwa kutumia vyombo vya habari, Magazeti, Redio, Televisheni, na Makala mbali mbali.
Juhudi hii ni katika kutekeleza agizo hilo ambalo tunaamini litaleta mwamko mpya hasa kwa Waislam kuijua hali waliyo nayo kwa sasa na wanatakiwa wafanye nini.
Na kuwasaidia wale watakaoshiriki katika kutoa maoni kwenye kamati ya kuratibu maoni ya uandishi wa katiba mpya.
Shukrani
Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani za dhati kwa wale wote waliochangia mada hii hadi kupatikana kwa maandiko haya katika umbo la kitabu. Mola Ajaalie Juhudi zao hizi ziwe katika Mizani ya Matendo yao mema siku ya Qiyaamah.
Mkusanyaji:
Shaykh Salim ‘Abdur-Rahiym Barahiyan, (L.L.B. Shari’ah, L.L.M. Shari’ah and Law)
P. O.BOX 1542,
TANGA
Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa Uislamu
SURA YA KWANZA
Kwa nini Mada hii?
Tuna sababu zifuatazo zinazotufanya tuzungumzie mada hii:
1. Ni katika kulingania dini yetu kwa Jihadi ya hoja na kuzuia Munkari (Maovu).
﴿فَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَجَاهِدْهُمْ بِهِ جِهَادًا كَبِيرًا﴾(الفرقان:٥٢ قال تعالى:
Amesema Allaah:
“Na wala usiwatii Makafiri na pigana nao Jihadi ya hoja ya (Quraan) Jihadi kubwa”. (Surat AlFurqaan: 52).
وقال تعالى:﴿ قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴾(يوسف:١٠٨).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Sema hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah kwa ujuzi mimi na yule aliyenifuata na Ametakasika Allaah na kila upungufu nami si katika washirikina”
(Surat Yuusuf: 108).
وقال صلى الله عليه وسلم:(من رأى منكم منكرا فليغيره بيده فإن لم يستطع فبلسانه فإن لم يستطع فبقلبه وذلك أضعف الإيمان)رواه مسلم.
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
“Atakaeona miongoni mwenu ovu lolote aliondoe kwa mkono yake, na kama hataweza basi na kwa ulimi wake na kama hataweza basi na aliondoe kwa moyo wake (alichukie) na hali hii (kulichukia kwa moyo) ni udhaifu mkubwa wa imani” (Imepokewa na Imaam Muslim).
عن النعمان بن بشير رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:(مثل القائم في حدود الله والواقع فيها كمثل قوم استهموا على السفينة فصار بعضهم أعلاها وبعضهم أسفلها وكان الذين في أسفلها إذا استقوا الماء مروا على من فوقهم فقالوا لو أنا خرقنا في نصيبنا خرقا ولم نأذي من فوقنا،فإن تركوهم وما أرادواهلكوا جميعا وإن أخذوا على أيديهم نجوا ونجوا جميعا).رواه البخاري.
Toka kwa Nu”umaan bin Bashiyr (Radhiya Allaahu ‘anhu) amepokea toka kwa Nabii (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) akisema:
“Mfano wa yule aliesimama katika mipaka ya Allaah na yule alievuka mipaka yake ni mfano wa watu walioingia kwenye Safina kwa kupiga kura na wakawa miongoni mwao juu ya ile Safina na wengine chini (inaashiria ukubwa wa hiyo Safina) ikawa wale waliokuwa chini wakitaka maji huyafuata kwa kupitia kwa wale wa juu, wakasema (kwa kushauriana): kama tungetoboa hukuhuku chini tungeyapata maji bila ya kuwaudhi wenzetu walio juu, kama wataachwa na matakwa yao hayo wataangamia wote na kama wakizuiwa wataokoka wote).”
(Imepokewa na Imaam Al-Bukhaariy).
قال الله تعالى:﴿ كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ)( آل عمران:١١٠)
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Mmekuwa Umma bora utokanao na watu mnaamrishana mema na mnakatazana mabaya na mnamwamini Allaah” (Surat Al-‘Imraan: 110).
2. Ni haki ya Kikatiba kwa kila Raia:
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania 18(1):
“Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa”
3. Ni wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa Raia wa nchi hii kuchangia maoni katika mchakato wa kuandikwa upya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:
Katika Gazeti la MWANANCHI la Jumamosi tarehe 1 Januari 2011:
“Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuanza mchakato wa kuandikwa katiba Mpya.Katika salamu zake za mwaka mpya kwa Taifa jana, Rais Kikwete alisema: “Nimeamua kuunda Tume Maalumu ya Katiba yaani Constitutional Review Commision. Tume hiyo itakayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbali mbali kutoka jamii yetu kutoka pande mbili za Muungano, alisema jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbali mbali ya watu wote, katika kutoa maoni wayatakayo kuhusu katiba ya nchi yao.”
4. Ni wajibu wetu kutoa Nasaha:
قال تعالى:﴿ وَإِنْ أَحَدٌ مِنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّى يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّهِ (التوبة:٦).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Kama mmoja yeyote katika washirikina atakuomba awe karibu nawe basi kuwa karibu nae ili apate kusikia maneno ya Allaah”
(Surat At-Tawbah: 6).
عن التميم الداري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:(الدين النصيحة.قلنا لمن يارسول الله.قال:لله ولكتابه ولرسوله ولأئمة المسلمين وعامتهم).رواه مسلم.
Imepokewa na Tamiym Ad-Daariy (Radhiya Allaahu ‘anhu),
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
“(Dini ni nasaha) tukasema kwa ajili ya nani ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu? akasema:kwa ajili ya Allaah na Kitabu Chake na Mtume Wake na kwa viongozi wa Waislamu na watu wote)”
(Imepokewa na Imaam Muslim).
وقال صلى الله عليه وسلم:(إذا استشار أحدكم أخاه فليشر عليه).رواه ابن ماجه.
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
“Atakapotaka ushauri mmoja wenu kwa ndugu yake basi amshauri”.
(Imepokewa na Ibn Maajah).
5. Kuwatanabaisha baadhi ya masheikh ambao mara baada ya Rais kutangaza mchakato wa Katiba mpya wakakurupuka na kutoa maoni kwamba wanataka mahakama ya Qaadhi (Kadhi) na nchi kujiunga na OIC na Ijumaa iwe ni siku ya mapumziko, na wameghafilika kwamba Katiba imewanyima haki zao za msingi na kubwa kuliko mahakama ya Qaadhi na OIC na siku ya Ijumaa. Na wengine kuona bado wakati wa kutoa maoni wamewausia WaIslamu wasiseme kitu wasubiri kamati ya kukusanya maoni itakayoundwa na Mheshimiwa Rais.
SURA YA PILI
Nini Maana Ya Katiba Ya Nchi? Kwa Mtazamo Usio Wa Kidini.
Katika nchi yoyote msingi wa uendeshaji wa nchi unategemea Katiba. Katiba ni sheria kuu au sheria mama katika nchi yoyote. Sheria nyingine zote zinategemea au zinatungwa kwa mujibu wa katiba, wakati mwingine katiba hutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kijamii kati ya watawala na wananchi (watawaliwa). Ni makubalianao ya wananchi husika juu ya ni jinsi gani taratibu za kanuni za uendeshaji wa mambo mbali mbali katika nchi yao unapaswa kuwa.
(Angalia kitabu HAKI Tolea la 5 Namba 4 Dec. 2002 Uk. 6).
Ni muafaka wa Kitaifa juu ya misingi mikuu ya kuendesha nchi.
(Maneno ya Pro.Shivji katika kongamano tarehe 15/1/2011Dar es Salaam.)
Maana ya katiba ya nchi kwa mtazamo wa Kiislamu
Sheria kuu na Sheria Mama katika nchi kwa mujibu wa Uislamu ni Qur-aan na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa sallam).
قال تعالى:﴿ فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ﴾.(النساء:٥٩).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Ikiwa mkikindana (kukhitalifiana) katika jambo lolote basi lilerejesheni (jambo hilo) kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake”
(Surat An-Nisaa: 59).
قال تعالى:﴿ وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُبِينًا ﴾(الأحزاب:٣٦).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Na haifai kwa muumini mwanamme au mwanamke pale atakapolitolea hukumu jambo lolote Mwenyezi Mungu na Mtume wake wawe na hiari katika kulitekeleza Jambo hilo, na anae muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakika amepotea upotevu wa wazi)”
(Surat Al-Ahzaab: 36).
Historia Ya Katiba Katika Nchi Zilizotawaliwa Na Makafiri
“Kwa ujumla nchi nyingi hasa zile zinazoendelea zina katiba zilizoandikwa.nyingi kati ya katiba hizo zilitungwa na kurekebishwa na watawala wa kikoloni, na nyingine zilitungwa baada ya makubaliano na tawala za kikoloni kabla ya kuondoka.Katiba hizo ni maridhiano ambayo yalilinda maslahi ya pande zote mbili:
(1)Tawala za kikoloni zilizokuwa zikiandika.
(2)Nchi iliyokuwa ikipata uhuru(Angalia Jarida la HAKI Toleo la 5 uk.7), (Angalia pia Shetani wa mwalimu uk.6):
"Katiba nyingi katika nchi zilizoendelea zina uhusiano na Katiba na Tawala za kikoloni.
Historia ya katiba hapa Tanzania pia ina uhusiano na tawala za kikoloni zilizokuwa zinatawala kabla ya uhuru".Angalia HAKI toleo la 5 uk.7(Kamati ya Msaada ya Kisheria).
Historia Ya Mabadiliko Ya Katiba Tanzania
1961Katiba ya kwanza ya uhuru iliyowekwa na waingereza (Independence Constitution).
1962Katiba ya Jamhuri (The Republic Constitution) iliitambua Tanganyika kama Jamhuri na ilipunguza madaraka ya Bunge(Imewekwa na Waingereza).
1965Iliwekwa katiba ya muda (The Interim Constitution)
1977Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitungwa na bunge maalum (Constitutional Assembly), (wananchi hawakuhusishwa).Angalia HAKI toleo la 5 uk.10).
Pr.Issa Shirji anabainisha haya pia katika kongamano la Katiba lililoandaliwa na wanataaluma wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Jumamosi tarehe 15/1/2011 angalia Gazeti la MWANANCHI uk.4 tarehe 16/1/2011.
Mabadiliko Makubwa Yaliyotokea Katika Katiba
1961Katiba iliruhusu mfumo wa vyama vingi,
Vyama vifuatavyo vilisajiliwa:TANU, United Tanganyika Party(UTP), African National Congress(ANC), The Peoples Democratic Party(PDP), Peoples Convertion Party(PNP), National Enterprise Party(NEP), All Muslim Nationalist Union of Tanganyika(AMNUT), African Independence Movement(AIM).
1963Halmashauri kuu ya TANU ilipitisha maamuzi kufanya Tanganyika kuwa nchi ya chama kimoja.
1965Sheria ya chama kimoja iliingizwa kwenye Katiba.1977Haki za binaadamu ziliingizwa rasmi katika Dibaji.
1984Katika katiba ya Jamhuri haki za binaadamu ziliingizwa rasmi katika katiba.
1992Katiba iliruhusu tena mfumo wa vyama vingi kwa shinikizo la nchi za kibeberu (kikafiri).
Katika kitabu: Elimu ya Demokrasia shirikishi (Kitabu kilichotolewa na CTP Dom uk.7) chasema hivi:
"Wanasayansi wa mambo ya siasa wanaelekea kukubali kwamba demokrasia ya vyama vingi imeingizwa toka nje kwa kutokana na masharti ya kupata misaada ya fedha".
Katiba Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Haibadiliki
قال تعالى:﴿ وَاتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنْ كِتَابِ رَبِّكَ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ﴾(الكهف:٢٧).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):”Nawasomee kilichoteremshwa kwako kwa wahyi (Ufunuo) katika kitabu cha Mola wako ambacho hayabadiliki maneno yake)” (Surat Al Kahfi: 27).
قال تعالى:﴿ وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ. لَا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنْزِيلٌ مِنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴾
(فصلت:٤١-٤٢)
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na hakika hiyo (Qur-aan) ni Kitabu kitukufu, hakiingiliwi na batili yoyote mbele yake wala nyuma yake imeteremka kutoka kwa Mwenye hekima ya hali ya juu na Mwenye kushukuriwa sana)”
(Surat Fusswilat: 41- 42).
SURA YA TATU
Mambo Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Yanayokwenda Kinyume Na Uislam
1. Mfumo Wa Demokrasia
Nini maana ya Democracy?
Ni neno lenye asili ya kigiriki (Demo – crates) yaani utawala wa watu.
"Ni mfumo wa kuendesha serikali ya watu iliyochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu, madaraka na mamlaka, ya mwisho ya serikali hiyo yako mikononi mwa watu"
(Angalia Jifunze Uraia kwa shule za msingi kitabu cha nne na S. A. Numisi uk. 10).
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, sehemu ya pili, Serikali na watu, sheria ya 1984 na.15, 16.6,
“Jamhuri ya muungano wa tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki za kijamii na kwa hiyo:
a) Wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii.
b) Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi serikali itawajibika kwa wananchi”
2. Mamlaka Ya Kutunga Sheria Yako Mikononi Mwa Watu Badala Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kifungu 64 (1):
“Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo yote yahusuyo Tanzania bara yatakuwa mikononi mwa bunge”
Kifungu 106 (3):
Madaraka yote ya kutunga sheria katika zanzibar katika mambo yote yasiyo mambo ya muungano yatakuwa mikononi mwa baraza la wawakilishi wa Zanzibar.
3. Mfumo Wa Kutenganisha Dini Na Mamlaka Ya Nchi (Siasa)
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kifungu 19 (2):
“Bila kuathiri sheria zinazohusika za jamhuri ya muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuia za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi”.
Katika katiba toleo la 2005 ibara ya 3:
3 (1) “Jamhuri ya muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa”.
4. Mfumo Wa Kufuata Siasa Ya Ujamaa Kwa Mujibu Wa Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano
Kifungu cha 9:
“Lengo la katiba hii ni kuendesha ujenzi wa jamhuri ya muungano na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu wa amani kutokana na kufuata siasa ya ujamaa na kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika jamhuri ya muungano”.
5. Mfumo Wa Kukataza Kuanzishwa Chama Cha Siasa Chenye Lengo La Kukuza Dini
Kwa mujibu wa katiba kifungu 20 (2):
“Kwa kujali masharti ya ibara ndogo (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na katiba au sera yake:
A) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya:
I) “imani au kundi lolote la dini”.
6. Sera Ya Kulazimisha Kila Raia Kufuata Na Kutii Katiba Ya Jamhuri Na Sheria Zake Hata Kama Zinakhalifu Shari”ah Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 26 (1):
“Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii katiba hii na sheria za jamhuri ya muungano”.
7. Kiongozi Wa Nchi (Rais) Kupewa Madaraka Ya Kuchupa Mipaka (Udikteta)
Ka mujibu wa katiba ya jamhuri kifungu 45 (1):
“Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:
A) kutoa msamaha kwa mtu yoyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote na aweza kutoa msamaha bila masharti au kwa masharti kwa mujibu wa sheria.
B) kumwachilia kabisa au kwa muda maalumu mtu yeyote aliyehukumiwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum.
C) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu.
D) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yote”.
8. Uhuru Wa Kubadilisha Dini Anayotaka
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 19 (1):
“Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake”.
9. Sera Ya Kugombea Uongozi Badala Ya Kugombewa
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 67 (3):
“Mtu hataweza kugombea uchaguzi kuwa mbunge wa kuwakilisha jimbo la uchaguzi katika uchaguzi mkuu wowote ikiwa wakati huo yeye amesimama katika uchaguzi kugombea kiti cha Rais, wala hataweza kugombea uchaguzi kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo wowote ikiwa yeye ni Rais”.
10. Mfumo Wa Vyama Vingi Vya Siasa
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 3 (1):
“Jamhuri ya muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa”.
11. Kiongozi Mkuu Wa Nchi (Rais) Kuwa Juu Ya Sheria
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 46:
(1): wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashtaka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
(2) wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa katiba hii, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosea kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais…
12. Matumizi Ya Mapambano (Jihadi) Yanakataliwa
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 20 (21):
“Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na katiba na sera zake:
(c) kinakubali na kufungamana na matumizi ya nguvu au mapambano kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa”.
13. Itikadi Ya Al-Walaa Wal-Baraa (Kupenda Kwa Ajili Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Na Kuchukia Kwa Ajili Ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Inavunjwa
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Haki ya Usawa, kifungu 12(4):
Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.
Kifungu 12 (5):
Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno “kubagua” maana yake ni kutimiza haja, haki, au mahitaji mengineyo kwa watu mbali mbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahali walipotokea, maoni ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali ya maisha kwa namna ambapo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa dhaifu au duni au kuwekewa vikwazo au masharti ya upingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa auwanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima isipokuwa kwamba neno “kubagua” halitafafanuliwa kwa maana ambayo “itazuia serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika jamii.
SURA YA NNE
Baadhi Ya Vipengele Na Maneno Yaliyomo Ndani Ya Katiba Vilivyopotoshwa Kwa Mtazamo Wa Uislamu
1. Neno Ibada: Limepewa Tafsiri Finyu
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 18 (2):
Bila kuathiri sheria zinazohusika za jamhuri ya muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada au kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi na shughuli za uendeshaji wa jumuia za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
2. Neno Halali
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 9:
Mamlaka ya nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:
(e)kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi, anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli ya halali inayompatia mtu riziki yake”.
3. Neno Usawa
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 13(1):
WATU WOTE MBELE YA SHERIA NA WANAYO HAKI, BILA YA UBAGUZI WOWOTE, KULINDWA NA KUPATA HAKI SAWA MBELE YA SHERIA.
Vile vile kifungu 12(1):
BINAADAMU WOTE HUZALIWA HURU NA WOTE NI SAWA.
4. Neno Haki Ya Kuishi
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu (1):
Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kwa uhuru.
Hii imetafsiriwa kwamba hata aliyeua asiuliwe kwa sababu ana haki ya kuishi.
5. Neno Haki Ya Kumiliki
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 24 (1):
“Bila kuathiri masharti ya sheria za nchi zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria”
Imefasiriwa kipengele hiki kwamba mtu ana haki ya kugawa urithi, atakavyo yeye maadam ni mali yake.
6. Kufutwa Adhabu Ya Viboko
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri kifungu 136(e):
Ni marufuku kwa mtu kuteswa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.
Mahakama kuu Dodoma katika kesi ya Thomas s/o Mjengi Vrs.R, Dodoma High Court Criminal appeal Na.28/1991 hapo tarehe 23/6/1992 ilihukumiwa kuwa adhabu ya viboko na adhabu ya kima cha chini cha kifungo cha miaka 30 kwa kosa la unyang”anyi ni kinyume cha Ibara ya 13(6) (e) ya Katiba yetu.
SURA YA TANO
Mtazamo Wa Uislamu Kuhusu:
1. Mfumo Wa Democracy
Ni matunda ya mapinduzi ya Kifaransa.
Demokrasia ni ushirikina Kwa sababu inampa Mwanaadamu Mamlaka na Madaraka ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).
Historia Ya Mapinduzi Ya Ufaransa
Kanisa la Ki-Roma lilitawala nchi za Ulaya kwa muda mrefu katika nchi za Ulaya. Kanisa lilidhulumu haki nyingi za raia wa Ulaya kwa jina la dini, hii ilipelekea kujitokeza wanaharakati kupinga dhulma hii ya kanisa, harakati hizo zilipelekea kufanyika Mapinduzi makubwa huko Ufaransa mwaka 1789 jambo ambalo limepelekea kanisa kuvuliwa madaraka ya Kisiasa na athari ya mapinduzi hayo ndiyo yaliyozusha mfumo wa:
1. Democracy: Watu ndio wenye mamlaka ya kila kitu.
2. Secularism: Kutenganisha Dini na Mamlaka ya nchi (Siasa).
Mfumo wa Demokrasia ni Ushirikina kwa sababu unampa mwanaadamu mamlaka ya Mungu.
قال تعالى:﴿ لَا تُشْرِكْ بِاللَّهِ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ﴾ (لقمان:١٣).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Wala usimshirikishe Allaah hakika ya ushirikina ni dhulma kubwa)”
(Surat al-Luqmaan:13).
وقال تعالى: ﴿ وَلِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴾ (آل عمران:١٨٩)
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Ni milki ya Allaah tu vilivyomo mbinguni na Ardhini na Allaah juu ya kila kitu ni muweza.”
(Surat al-‘Imraan: 189).
2. Ni Nani Mwenye Haki Ya Kuweka Sheria?
قال تعالى: ﴿ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ﴾ (الأعراف:٥٤).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Eleweni ni miliki yake yeye tu (Allaah) kuumba na kuamrisha)”
(Surat Al-A’araaf: 54)
وقال تعالى: ﴿ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ﴾ (يوسف:٤٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“(Hukumu ni ya Allaah (peke yake) ameamrisha musiabudu chochote isipokuwa yeye tu)”Surat Yusuf: 40).
وقال تعالى: ﴿ اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَهًا وَاحِدًا لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴾ (التوبة:٣١).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“(Wamewafanya (Mayahudi na manaswara) wanazuoni wao na watawa wao na ‘Iysa mtoto wa Maryamu kuwa ni miungu kinyume na Allaah, na hali ya kuwa hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Mungu mmoja hakuna mungu mwingine anaepasa kuabudiwa isipokuwa Yeye tu utakasifu ni Wake na kila kile ambacho wanachomshirikisha nacho)”
(Surat At-Tawbah: 31)
Katika Aya hii, Mayahudi na Manaswara wamelaumiwa kwa kuwageuza wanachuoni wao na watawa wao kuwa ni Miungu kwa sababu waliwahalalishia yaliyoharamishwa na Mola na wao wakawatii na waliwaharamishia yaliyoharamishwa na Mola na wao wakawatii. Kazi ya kuweka Sheria ni ya Allaah tu peke yake sio ya Mtu wala Bunge.
وقال تعالى: ﴿ أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْمًا لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴾ (المائدة:٥٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Hivi wanataka wahukumiwe na hukumu ya Kijahili?! Na ni Nani (hakuna) mwenye hukumu ya sawa (zaidi ya Allaah) kwa watu wenye kuyakinisha?”
(Surat Al-Maaidah: 50).
Sheria Ya Ndoa Ya 1971 Iliyotungwa Na Binaadam Ilivyokiuka Shari’ah Za Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Za Ndoa
Kifungu 160:
Mwanamme na mwanamke wakiishi pamoja kwa muda wa miaka 2 mfululizo huweza kuchukuliwa ni mke na mme mbele ya sheria japokuwa hawakuwahi kufunga ndoa.
Ndoa hii haitambuliwi katika Uislam bali inahesabiwa ni uzinifu.
قال تعالى: ﴿ وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا ﴾ (الإسراء:٣٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Musiikaribie zinaa hakika hiyo (zinaa) ni uchafu na njia mbaya”
(Surat Al-Israa 32).
Kifungu cha 18 (1):
Iwapo mwanamme na mwanamke wanaotaka kuoana, itawabidi kutoa taarifa ya nia yao ya kuoana kwa msajili au ofisa wa usajilishaji kwa siku 21 kwa uchache, kabla ya siku wanayotaka kuoana kufika.
Kifungu Cha 114:
Inakatazwa katika kifungu hiki mtu kuoa au kuolewa na mzazi wake, mtoto au mjukuu wake, kama ni dada yake, mama au shangazi au baba na mjomba wake, baba au mama wa kambo na mwanae aliyemfanya mwanae (adopted child).
Katika Uislam anaelelewa anaweza kuolewa na mwenye kumlea.
Sheria ya Kiislamu Haiwezi Kuvunja Sheria ya Ndoa 1971
Kwa Mujibu wa Sheria iliyotungwa na Binaadam:
(Cap. (Kiambatanisho 453: The rules of cust Omary law and the rules of Islamic law shall not apply in regard to any matter provided for in the law of Marriage Act 1971 (Angalia Sheria ya Kiislamu ya Mirathi na Wasia – na Mahmoud A. Sameja) uk. 37
Paragraph 1 of Government Notice No.196 of 1971 made under Sect.102 of The Law of Marriage Act Categorically states that:
The above Boards (Marriage Conciliation Boards) must comply with the provisions of the law of marriage Act and any other provisions hereunder.
(Angalia Bakwata and the Administration of Islamic law: Problems: A case study of DSM by Mohammad Awadh).
Tafsiri (Isiyo Rasmi):
Kanuni za sheria za kimila na kanuni za sheria ya Kiislam haitoruhusiwa kutumika katika suala lolote linalohusiana na sheria za Ndoa ya mwaka 1971.
((Angalia Sheria ya Kiislamu ya Mirathi na Wasia – na Mahmoud A. Sameja) UK.37).
Kipengele cha 1 cha Tangazo la serikali namba 196 ya 1971 iliyotungwa chini ya kifungu cha 102 cha sheria ya Ndoa katika mfululizo inayosema kwamba:
Kamati tajwa hapo juu (Kamati za usuluhishi wa Ndoa) lazima zifuate vifungu vya sheria ya Ndoa na vipengele vingine.
(Angalia Bakwata and the Administration of Islamic law: Problems: A case study of DSM by Mohammad Awadh).
Kifungu 153 (1):
Mtu yeyote ambaye ni mmoja wa wafunga ndoa au anaeshiriki kwenye shughuli ya ndoa iwapo:
(a) mke anaekusudiwa yuko chini ya umri wa miaka 18 na idhini ya ndoa kama inavyotakiwa na fungu la 17 haikutolewa au;
(b) taarifa ya nia ya kufunga ndoa, kama inavyotakiwa na fungu la 18, haikutolewa.
Basi mtu huyu atakuwa ni mkosa na atakapoonekana kuwa ana hatia astahiki kifungo kwa muda usiozidi miezi sita.
Kwa Makusudio ya fungu la 148 mpaka 155 kushiriki kwa shughuli ya ndoa yake:
a. Kufungisha ndoa hiyo, au
b. Kutoa idhini katika ndoa hiyo
c. Kuwa shahidi wa ndoa hiyo
Wakati sheria hizi zinatungwa 1971 BAKWATA ilishindwa kutetea Uislam na moja ya malengo ya kuundwa kwake yamebainishwa ndani ya katiba yao:
MADHUMUNI 9,
“Madhumuni ya Baraza Kuu la waislam Tanzania yatakuwa haya yafuatayo:
2. kusimamia na kutetea haki za Msingi za Waislam nchini na kukemea mambo yanayoleta kero kwa waislam”
Je Sheria ya Ndoa ya Kiislam sio katika haki za kimsingi za waislam? Mbona BAKWATA imekaa kimya juu ya hili?
3. Mfumo Wa Kutenganisha Dini Na Dola (Mamlaka/Utawala) Wa Nchi
Uislam hautenganishi mamlaka ya nchi (siasa) na dini kwani Dini inatuongoza waislam katika kila kipengele cha maisha ibada, jamii, siasa uchumi n.k.
قال تعالى: ﴿قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴾ (الأنعام:١٦٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Waambie Swalah yangu na ibada zangu (kuchinja kwangu) na uhai wangu na kifo changu ni kwa ajili ya Allaah Mola wa viumbe wote”
(Surat Al-An’aam: 162).
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) na Makhalifa wake walikuwa ni viongozi wa mamlaka ya Dini na Nchi (siasa).
Kutekeleza Sheria za Jinai ni katika sehemu ya Dini
قال تعالى: ﴿ الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا مِئَةَ جَلْدَةٍ وَلَا تَأْخُذْكُمْ بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّهِ إِنْ كُنْتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآَخِرِ﴾ (النور:٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanaume wapigeni kila mmoja wao mijeledi mia moja wala isiwachukueni huruma katika kutekeleza Dini ya Mwenyezi Mungu ikiwa (kweli) mnamuamini Allaah na siku ya mwisho”
(Surat An-Nuur: 2).
Kutekeleza sheria za jinai ni sehemu ya dini na imani, hii ni hoja dhidi ya wale waislam wanaotaka u-Qaadhi wa ndoa, talaka, mirathi wakfu, malezi na wasia tu na sio u-Qaadhi wa shari’ah zote.
Kiongozi Wa Nchi Ya Kiislam Ni Kiongozi Wa Kisiasa Pia
وقال أبوالحسن الماوردي الشافعي رحمه الله (ﺕ٤٣٠):الإمامة موضوعة الخلافة النبوة في حراسة الدين وسياسة الدنيا وعقدها لمن يقوم بها في الأمة واجب بالإجماع(الأحكام السلطانية\ص ٥).
“Na amesema Abu Al-Hasan Al-Mawardiy mfuasi wa Imaam Ash-Shafi’iy (aliekufa mwaka 430 H.), Uongozi ni shemu ya Ukhalifa wa utume Katika kulinda Dini na siasa ya dunia na kuusimamisha kwa yule anaesimamia hilo katika umma ni wajibu kwa makubaliano ya wanazuoni.
(Kitabu Al-Ahkaam As-Sultaaniyyah, uk. 2).
قال ابن تيمية رحمه الله:(فالواجب اتخاذ الإمارة دينا وقربا يتقرب بها إلى الله فإن التقرب إليه فيها بطاعته وطاعة رسوله من أفضل القربات:(السياسة الشرعية\١١٩).
Amesema Shaykh wa Uislamu Ibnu Taymiyyah (Allaah Amrehemu):
‘‘Basi ni wajibu kuweka uongozi kwa ajili ya Dini na kujikurubisha kwa Allaah hakika kujikurubisha kwa Allaah kwa kumtii na kumtii Mtume wake ni katika vikurubisho (Ibada) bora.’’
(Kitabu As-Siyaasatu Ash-Shar’iyah, uk, 119).
Viongozi Wa Majimbo Walikuwa Wanasiasa Zama Za Makhalifa
ولى الفاروق عمار بن ياسر على الكوفة،ثم كتب أهلها شكوى ضد عمار بأنه ليس بأمير ولا يحتمل،فاستدعى عمر رضي الله عنه عمار بن ياسر رضي الله عنه فأقبل ومعه جمع من أهل الكوفة فسألهم عمر فقالوا:هو والله غير كاف ولا يجزأ ولا عالم بالسياسة ولا يدري علام استعملته.فسأله عمر بحضورهم عن أمور ولايته ممتحنا إياه لمعرفة مدى خبرته في الحكم.فلم يجب بما يرضى عمر فعزله.(تاريخ الطبرى ج\٤،ص ١٦٢).
(Al Faruuq ‘Umar Ibn Al Khattwaab alimpa utawala ‘Ammaar Bin Yaasir huko Kuuufah, kisha watu wake wakamshitaki kwamba si kiongozi anaefaa na wala si mvumilivu, akamwita ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) afike kwake akafika akiwa na kundi la watu wa Kuufah, akawauliza ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) wakasema, huyu tunaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa wala hafai wala hajui siasa jambo gani umemtawalisha nalo, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamuuliza mbele yao kuhusu utawala wake akimjaribu ili ajue kiwango cha uelewa wake katika uongozi akawa hakutoa majibu yaliyomkinaisha ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) na akamvua madaraka).
(Kitabu cha Taariykh At-Twabariy, juzuu ya 4, uk. 162).
Kauli Ya Aboud Jumbe:(Rais Mstaafu Wa Zanzibar Na ‘‘Makamu Wa Mwenyekiti Wa CCM Mstaafu).
Kwa Uislam basi dini haiwezi kutenganishwa na siasa kwa sababu ni sehemu ya maisha.’’
(Angalia The Partnership uk.131).
Wakristo Wanakiri Kwamba Uislam Ni Njia Kamili Ya Maisha
Katika kitabu “KUWASHIRIKISHA WAISLAMU UPENDO WA MUNGU na Bill Danett UK 21.
“Uislam unaingia katika mambo yote ya maisha”
“Ni muhimu kufahamu kuwa uislam ni njia ya maisha yote. Waislam huamini kuwa ummah wao ndio bora ulio inuliwa kwa ajili ya binadamu (Quraan 3: 110), maongozi ya ummah huo yanathibitika katika uadilifu, usafi, ukarimu, na uhusiano bora katika familia. Uislamu hukusiana na mambo yote ya maisha: dini, maadili, jamii, utamaduni, uchumi, na siasa. Hutawala kila dakika ya maisha yao saa ishirini na nne kila siku tangu kuzaliwa hadi kufa. Mwislamu si mtu binafsi tu, bali mshiriki katika jamii iliyo na uhusiana wa karibu sana na ndani ya jamii hii, ushiriki pia katika familia yenye uhusiano uliyo wa karibu hapa zaidi.
(Kimechapwa 1992 na life challenge Africa s.l.p 50770, city square 00200, Nairobi, Kenya).
Wakristo Nao Pia Wanakiri Kwamba Uislam Haukutenganisha Dini Na Siasa Tangu Zamani
Anasema Fredrick Fredolin Portmann katika kitabu chake: DINI MBALI MBALI NA UTUME WETU.
“Zamani Quraan ilikuwa sheria ya maisha yote si ya dini tu, ila pia ya serikali na siasa’’ uk. 30
Mfumo wa kutenganisha dini na siasa (mamlaka ya nchi) ni wa kikristo, na Waingereza (wakristo) walipoasisi katiba ya nchi hii ndio walituwekea msingi huu, Katika Biblia Yesu amenukuliwa akisema,
“Basi mpeni Kaizari vilivyo vyake na vya Mungu vilivyo vyake (Matayo 22:20) na amesema ufalme wangu sio wa ulimengu huu’’ (Yohana 18:36)
katika Kitabu Wana wa Ibrahim UK. 156, chasema hivi:
a. Kwa waislamu mungu na kaysar ni mmoja, yaani asili ya uislamu ilitaka kuchanganya dini na utawala, muhammad alianzisha ujamaa wa pekee ukiwa na sheria ambamo kuna siasa na utawala, na dini na sheria mbali mbali kuhusu yatima, urithi, ndoa, uhusiano na wanafiki, na wapagani, usafi na unajisi, vita na jihadi kisasi, namna ya kuwaendea mahaini na watumwa na wanawake.hayo yote yanaitwa “hudud Allaah” yaani sheria za mungu (kuran 2:188) ni kama mipaka ambayo hairuhusiwi kuivuka”.
b. Wakristo waliotaka utawala wa kidini katika karne zilizopita hawakufanya vile kwa agizo la yesu, kwa sababu agizo lake ni hili: ”vya kaesari, mpeni kaesari, na vya mungu mpeni mungu (lk 20: 25) maana yake wapeni watawala heshima na utii wanayostahili katika mambo ya dunia, na mpeni mungu heshima na utii katika mambo ya roho. Yesu hataki kuchanganya ufalme wa dunia na ufalme wa mungu…dini ni tofauti na serikali, kwa vile dini inaweza kuwashauri watawala ili watawale vyema (ef:6:9) lakini hautaki kutawala badala yao… uk. 158.
4. Siasa Ya Ujamaa
Maana ya Ujamaa ni mfumo wa fikra za kisiasa na uchumi ambazo zimejengwa katika kuamini kwamba kila mtu ana haki sawa katika kupata sehemu ya utajiri wa nchi na kwamba serikali ndiyo inayomiliki njia zote kuu za uchumi.
Uislam haujapinga mtu binafsi kujitajirisha maadamu anatoa Zakaah.
قال تعالى: ﴿ لِلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِمَّا اكْتَسَبُوا وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِمَّا اكْتَسَبْنَ ﴾ (النساء:٤).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Wanaume wana fungu katika mali walizochuma na wanawake wana fungu katika mali walizochuma”
(Surat An-Nisaa: 4).
وقال تعالى: ﴿ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآَتُوا الزَّكَاةَ﴾ (البقرة:٤٣).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Na simamisheni Swalah na toeni Zakaah.’’
(Surat Al-Baqarah: 43).
وقال تعالى: ﴿ أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَةَ رَبِّكَ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُمْ مَعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِيَتَّخِذَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا سُخْرِيًّا وَرَحْمَةُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِمَّا يَجْمَعُونَ ﴾ (الزخرف:٣٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)
“Je wao ndio wanaogawa Rehema za Mola wako?! Sisi ndio tuliogawa maisha yao hapa duniani na tukawanyanyua baadhi yao kuwazidi wengine kwa daraja nyinyi ili wawafanye baadhi yao wengine kuwa watumishi wao, na rehema ya Mola wako bora kuliko kile wanachokikusanya”
(Surat Az-Zukhruf: 32).
وقال صلى الله عليه وسلم:(فأعلمهم أن الله فرض عليهم صدقات تأخذ من أغنيائهم وترد على فقرائهم)(رواه البخاري).
Na amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam): ‘‘Na waelimishe kuwa Allaah Amewawajibishia Sadaka (Zakaah) ambayo huchukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kurudishwa kwa masikini wao.’’
(Ameipokea Imaam Al-Bukhaariy).
Uislam hauna mipaka ya kujitajirisha maadamu chumo ni la halali, na hakuna sera za kutaifisha mali za watu kwa dhulma.
قال تعالى: ﴿ وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُمْ بَيْنَكُمْ بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا فَرِيقًا مِنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ﴾ (البقرة:١٨٨).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na wala msile mali zenu kati yenu kwa batili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali za watu kwa dhambi na nyinyi mnajua”
(Surat Al-Baqarah: 188).
Kwa siasa ya ujamaa watu walidhulumiwa haki zao kwa uonevu kwamba ni mabepari na mabwenyenye, makabaila na wanyonyaji kinyume hata na katiba ya nchi kifungu No.22 (2):
Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1): ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili.
5. Mfumo Wa Kukataza Kuanzisha Chama Cha Siasa Chenye Lengo La Kukuza Dini
Katika Uislamu mfumo huu haukubaliki kwa sababu Dini ndio inayotuongoza katika kila kitu amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
قال تعالى:﴿ شَرَعَ لَكُمْ مِنَ الدِّينِ مَا وَصَّى بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَى وَعِيسَى أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ﴾(الشورى:١٣).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
‘‘Amekuwekeeni shari’ah itokanayo na Dini aliyomuusia Nuuh na ambayo tumekuteremshia wahyi kwako na tuliyomuusia Ibraahiym na Muusa na ‘Iysa kwamba musimamishe Dini wala msifarikiane (kwenye Dini).’’
(Surat Ash-Shuuraa: 13).
وقال تعالى:﴿ قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ﴾(يوسف:١٠٨).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
‘‘Waambie hii ndio ndio njia yangu nalingania kwa Allaah kwa ujuzi)”
(Surat Yuusuf: 108).
Kutangaza Dini ni wajibu wa kila Muislam akiwapo mwanasiasa, lakini katiba inazuia mwanasiasa kusimamisha dini.
6. Sera Ya Kulazimisha Kila Raia Kufuata Na Kutii Katiba Na Sheria Za Nchi Hata Zikikhalifu Shari’ah Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) (Kitabu Na Sunnah)
Waislamu wanalazimika kufuata shari’ah za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na sio za twaghuut.
قال تعالى:﴿ أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آَمَنُوا بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنْزِلَ مِنْ قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَنْ يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَنْ يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا﴾(النساء:٦٠).
Amesema Allaah: (Subhaanahu wa Ta’ala):
‘‘Hivi hauwaoni wale ambao wanadai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako (kisha) wanataka wahukumiwe na Twaghuti (asiekuwa Allaah) hali ya kuwa wameamrishwa kumkufuru huyo (Twaghuti) na anataka Shaytwaan kuwapotosha upotoshi wa mbali)”
(Surat An-Nisaa: 60).
Waislam tunaamrishwa kufuata Qur-aan:
وقال تعالى:﴿ وَهَذَا كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴾(الأنعام:١٥٥).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na hiki Kitabu Tumekiteremsha chenye Baraka kifuateni na mcheni (Allaah) ili mpate kurehemewa”
(Surat Al-An’aam: 155).
وقال تعالى:﴿ ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَى شَرِيعَةٍ مِنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴾(الجاثية:١٨).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Kisha tukakufanya ufuate shari’ah itokanayo na amri (ya Allaah) ifuate shari’ah hiyo wala usifuate matamanio ya wale wasiojua)”
(Surat Al-Jaathiyah: 18).
وقال تعالى:﴿ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَى أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ﴾(الأنعام:١٢١).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na hakika Mashaytwaan huwatia maneno wapendwa wao ili wakujadilini (kwa kupinga) na kama mkiwatii hakika yenu nyinyi mtakuwa ni washirikina”
(Surat Al-An’aam: 121).
وقال صلى الله عليه وسلم: لا طاعة المخلوق في معصية الخالق(رواه البخاري)
Na amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
”Hakuna kumtii kiumbe kwenye jambo la kumuasi Muumba”
(Ameipokea Imaam Al-Bukhaariy).
لما بايع المسلمون أبابكر الصديق رضي الله عنه بيعة .... في السقيفة جلس في اليوم التالي للبيعة العامة ثم قام خطيبا في الناس فحمد الله وأثنى عليه بما هو أهله ثم قال:أما بعد ايها الناس فإني قد وليت عليكم ولست بخيركم فإن أحسنت فأعينوني وإن أسأت فقوموني الصدق أمانة والكذب خيانة والضعيف فيكم قوي عندي حتى آخذ علته إن شاء الله وإن القوي فيكم ضعيف حتى آخذ منه الحق إن شاء الله لا يدع القوم الجهاد في سبيل الله إلا جربهم الله بالذل ولا تشيع الفاحشة في قوم إلا عمهم الله بالبلاء اطيعوني ما أطعت الله ورسوله فإن عصيت الله ورسوله فلا طاعة لي عليكم.(السيرة لابن كثير ج\٣ ص ٤٩٢ ط\دار المعرفة)
“Walipomba’ii (kumkubali kuwa kiongozi) waislamu Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika bustani alikaa siku ya pili yake ili aba’iiwe na watu wote kisha akasimama na kuhutubu akasema: ‘‘Baada ya hayo, enyi watu mimi nimetawalishwa kuwa mtawala wenu lakini sio mimi ndio mbora wenu kama nikifanya vizuri nisaidieni na kama nikifanya vibaya nirekebisheni, ukweli ni amana na uongo ni hiyana dhaifu wenu kwangu ndio mwenye nguvu mpaka nimrejeshee haki yake, na mwenye nguvu kwenu ni dhaifu kwangu mpaka nichukue haki yake, In-shaa Allaah., hawatoacha watu jihadi katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) isipokuwa Mwenyezi Mungu huwapa udhalili na hayataenea maovu kwa watu isipokuwa Allaah Atawanezea mabalaa. Nitiini muda nitakapokuwa namtii Allaah na Mtume Wake na kama nikimuasi Allaah na Mtume Wake msinitii” (Kitabu Ibn Kathiyr Juzuu 3, uk. 492, chapa ya Daar Al Maarifah).
قال تعالى:﴿ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنْكُمْ﴾(النساء:٥٩).
Na amsema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“(Enyi ambao mlioamini mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume na waliotawalia mambo miongoni mwenu”
(Surat An-Nisaa: 59).
عن ابن عمر رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:(على المرء المسلم السمع والطاعة فيما أحب وكره إلا أن يؤمر بمعصية فإذا امر بمعصية فلا سمع ولا طاعة)(متفق عليه).
Na amepokea Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) amesema: ”Inampasa Muislamu kusikia na kutii kwenye kitu anachokipenda au anachokichukia isipokuwa akiamrishwa Maasi kama akiamrishwa Maasi asisikilize wala kutii” (Wameipokea Al-Bukhaariy na Muslim).
7. Kiongozi Wa Nchi Kupewa Madaraka Ya Kusamehe Au Kupunguza Adhabu
Katika Uislam kiongozi anaweza kusamehe au kupunguza adhabu za taaziyr tu na hana uwezo wa kusamehe huduud na haki za watu.
أسامة بن زيد شفع لدى رسول الله صلى الله عليه وسلم في المرأة المخزومية:(قرشية التي سرقت فقال صلى الله عليه وسلم:ياأسامة أتشفع في حد من حدود الله ثم قام فقال:إنما هلك الذين من قبلكم أنهم كانوا إذا سرق فيهم الشريف تركوه،وإذا سرق الضعيف اقاموا عليه الحد وأيم اتلله لو أن فاطمة بنت محمد سرقت لقطعت يدها.(رواه البخاري).
“Swahaba Usaamah bin Zayd alitaka alimwombea kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) mwanamke wa koo la Makhzumiy litokanalo na kabila la ma-Quraysh mwanamke ambae aliiba. Mtume akamwambia Usama: ‘‘Ewe Usaamah unafanya maombezi kwenye Had (Adhabu) miongoni mwa Huduud za Allaah, kisha akatoa khutbah Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: ‘‘Hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu ilkuwa akiiba mtukufu miongoni mwao humuacha (bila ya Adhabu) na kama akiiba dhaifu humsimamishia Had (Adhabu) juu yake. Naapa kwa Allaah hata kama Faatwimah bint Muhammad (yaani binti yake) akiiba nitakata mkono wake”
8. Uhuru Wa Kubalidisha DiniKatika Uislamu mtu akishakuwa Muislamu basi hana uhuru kubalidilisha dini na akibalidisha basi atatakiwa arudi na akikataa basi anauawa.
قال صلى الله عليه وسلم:(من بدل دينه فاقتلوه)(رواه البخاري).
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
”(Mwenye kubadili Dini yake (Uislamu) basi muueni)” (Ameipokea Al-Bukhaariy).
قال تعالى:﴿ وَمَنْ يَرْتَدِدْ مِنْكُمْ عَنْ دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآَخِرَةِ وَأُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾(البقرة:٢١٧).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Mwenye kuacha Dini yake miongoni mwenu na akafa hali ya kuwa ni kafiri hao matendo yao yatakuwa yameporomoka duniani na akhera na hao ni watu wa motoni watakaa humo milele”
(Surat Al-Baqarah: 217).
ويقول رسول الله صلى الله عليه وسلم:(لا يحل دم امرئ مسلم يشهد أن لاإله إلا الله وأني رسول الله إلا بإحدى ثلاث:الثيب الزاني،والنفس بالنفس والتارك لدينه المفارق للجماعة(رواه البخاري).
Na anasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
”Si halali (haramu) kuimwaga damu ya Muislamu yeyote mwenye kushuhudia kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na mimi ni Mtume wa Allaah isipokuwa kwa kufanya moja ya mambo matatu: mzinifu alieoa au kuolewa, aliyeua, aliyeiacha Dini yake mwenye kuacha umoja”
(Ameipokea Al-Bukhaariy).
Shubha: (Hoja ya wapinzani)
Msimano huu wa Uislam ni kinyume na Tangazo la ulimwengu la Haki za Binaadam la mwaka 1945 kifungu 18(b) kwa mtu ana uhuru wa kubalidisha dini anayotaka
Jawabu:
La kushangaza katika nchi nyingi za kisekula mtu akifanya kosa la uhaini (treason) anauliwa kwa sababu tu amekwenda kinyume na nidhamu ya Dola kwa lengo la kugeuza nidhamu ya utawala uliopo, mbona Uislamu unalaumiwa kwa jambo ambalo likifanywa na wengine hawalaumiwi?
9. Sera Ya Kuupapatikia Uongozi Na Kuugombania
Katika Uislam ni Haramu mtu kuomba au kupapatikia uongozi.
عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه قال:(دخلت على النبي صلى الله عليه وسلم أنا ورجلان من الأشعريين فقال أحدهما يارسول الله أمرنا على بعض ما ولاك الله وقال الآخر مثل ذلك فقال:إنا لا نولي على هذا العمل أحدا سأله ولا أحد حرص عليه قال صلى الله عليه وسلم لعبد الرحمن بن صخرة :ياعبدالرحمن لا تسأل الإمارة فإنك إن أعطيتها عن مسألة وكلت إليها وإن أعطيتها من غير مسألة أعنت عليها(رواه مسلم).
Imepokewa kutoka kwa Abuu Muusa Al-Ash’ariy (Radhiya Allaahu ‘anhu) Amesema: ”Niliingia kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) mimi na watu wengine wawili watokanao na Al-Ash’ariy (koo/kabila) mmoja wao akasema ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu nipe uongozi kwenye baadhi ya vile alivyokutawalisha Allaah, na yule mwingine akasema hivyo hivyo. Akasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) sisi hatumpi kazi hii ya uongozi mtu yeyote yule aliyeiomba au mtu aliyepupia, akasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) kwa Abdur-Rahmaan Ibn Swakhrah (Radhiya Allaahu ‘anhu): Ewe Abdur-Rahmaan usiuombe uongozi kwani wewe ukipewa huo uongozi kwa kuuomba utaachiwa bila kusaidiwa na kama ukipewa uongozi bila ya kuuomba utasaidiwa”
(Ameipokea Muslim).
عن أبي هريرة رضي الله عنه:أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:إنكم ستحرصون على الإمارة وستكون ندامة يوم القيامة(رواه البخاري).
Amepokea Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) amesema:
”Hakika nyinyi mtapapia uongozi kisha itakuwa ni majuto kweni siku ya Qiyaamah”
(Ameipokea Al-Bukhaariy).
10. Mfumo Wa Vyama Vingi Vya Kisiasa
Katika Uislam vyama ni viwili (2) tu chama cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na chama cha Shaytwaan.
Si ruhusa katika Uislam kuunda makundi ambayo hujiita vyama vya upinzani kazi yao ni kupinga serikali iliyo madarakani haijawahi kutokea tangu zama za Makhalifa hadi Khalifa wa Mwisho hakujawa na mfumo wa vyama vingi.
Sera ya vyama vingi umeasisiwa Firauni na hatimae imeletwa na Makafiri hapa nchini.
قال تعالى:﴿ إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَائِفَةً مِنْهُمْ﴾(القصص:٤).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hakika Firauni alijikweza katika hii Ardhi na kuwagawa watu wake makundi tofauti na akawadhoofisha baadhi yao”
(Surat Al-Qaswasw: 4).
Katika kitabu: ELIMU YA DEMOKRASIA SHIRIKISHI (Kitabu cha 4 kimotolewa na C.P.T. DSM UK.7:
“Wanasayansi wa mambo ya siasa wanaelekea kukubali kwamba demokrasia ya vyama vingi imeanzishwa toka nje kwa kutokana na shinikizo la masharti ya kupata misaada ya fedha.’’
Uislamu Unatutaka Waislam Tuwe Kitu Kimoja
قال تعالى:﴿ وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا﴾(آل عنران:١٠٣).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Shikamaneni na kamba (Dini) ya Mwenyezi Mungu nyote wala msitofautiane”
(Al-‘Imraan 103).
وقال تعالى:﴿ إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ﴾(الأنعام:١٥٩).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Hakika wale ambao wameacha Dini zao na kuwa makundi makundi wewe hauhusiki nao kwa lolote.”
(Surat Al-An’aam: 159).
11. Kiongozi Wa Nchi (Rais) Kuwa Juu Ya Sheria
Katika Uislam mtawala na mtawaliwa wote wako sawa katika sheria.
قال صلى الله عليه وسلم:(لو أن فاطمة بنت محمد سرقت لقطعت يدها)(رواه البخاري).
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam): ”Hata kama Faatwimah mtoto wa Muhammad akiiba nitakata mkono wake”
(Imepokewa na Al-Bukhaariy).
Kisa cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) alipowaaga Waislam
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) wakati wa maradhi yake aliyokufa nayo alitoka nje kwa kutolewa na Al-Fadhli bin ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) na ‘Alliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kuwekwa juu ya mimbari kisha akasema:
(أيها الناس من كنت جلدت له ظهرا فهذا ظهري فليستقد منه ومن كنت شتمت له عرضا فهذا عرضي فليستقد منه ومن أخذت له مالا فهذا مالي فليأخذ ماله ولا يخشى الشحناء من قبلي فإنها ليست من شأني ألا وإن أحبكم إلي من أخذ مني حقا إن كان له أو حللت فلقيت ربي وأنا طيب النفس ثم نزل فصلى الظهر ثم رجع إلى المنبر فعاد لمقالته الأولى(الكامل في التاريخ ج٢ ص ١٣٢ لابن الآثير).
“Enyi watu yoyote yule ambaye nimemchapa mgongo wake basi huu ni mgongo wangu na aje kulipiza kisasi, na kwa yule ambaye nimemvunjia heshima yake basi hii ni heshima yangu na aje kulipiza kisasi na yule niliyemchukulia mali yake basi hii ni mali yangu na aje kuchukua haki yake, na wala usiogopwe uadui toka kwangu kwani hilo sio katika shani yangu, na mjue kuwa kipenzi zaidi kwangu katika nyinyi ni yule aliechukua haki yake toka kwangu na akanisamehe na nikakutana na Mola wangu hali ya kwamba nafsi yangu imetakasika, kisha akashuka na kuswali Adhuhuri kisha akarejea kutamka maneno yake ya mwanzo.
(Angalia Kitabu Al-Kaamil Fiy Taariykh Juzuu 2, uk. 132 cha Ibn Athiyr).
Kisa Cha Khalifa ‘Alliy Alipomushtaki Yahudi Mbele Ya Qaadhi Shurayh
Ambapo Khalifa alipoteza ngao yake ya vita, kisha akaiona kwa Myahudi hakuichukua kutoka kwake bali alimshitaki kwa Qaadhi mkuu Shurayh, akakosa Khalifa ushahidi, akahukumu Qaadhi Shurayh kuwa ile ngao ni ya Yahudi, na hivyo Yahudi kuwa ni mshindi katika kesi hii.
عَنْ أَبِى فِرَاسٍ قَالَ: خَطَبَنَا عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ رَضِىَ اللَّهُ عَنْهُ فَقَالَ فِى خُطْبَتِهِ: أَلاَ وَإِنِّى لَمْ أَبْعَثْ إِلَيْكُمْ عُمَّالِى لِيَضْرِبُوا أَبْشَارَكُمْ وَلاَ لِيَأْخُذُوا أَمْوَالَكُمْ وَلَكِنْ بَعَثْتُهُمْ لِيُعَلِّمُوكُمْ دِينَكُمْ وَسُنَنَكُمْ فَمَنْ فُعِلَ بِهِ غَيْرُ ذَلِكَ فَلْيَرْفَعْهُ إِلَىَّ فَأُقِصَّهُ مِنْهُ. من كتاب السنن الكبرى للبيهقي.
Imepokewa Na Abuu Firaasi Amesema:
”Alihutubu ‘Umar Ibn Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema katika hotuba yake, ‘‘Eleweni kuwa mimi sijawatuma kwenu viongozi wangu ili wawapige na kuchukua mali zenu lakini nimewatuma kwenu ili wawafundisheni Dini yenu na Sunnah zenu atakaefanyiwa kinyume na hivyo basi ashitaki kwangu na nitamlipizia kisasi kwa huyo kiongozi”.
(As-Sunanu Al-Kubraa ya Imaam Al Bayhaqiy).
عَنْ أَبِى سَعِيدٍ الْخُدْرِىِّ قَالَ: بَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ –صلى الله عليه وسلم يَقْسِمُ شَيْئًا أَقْبَلَ رَجُلٌ فَأَكَبَّ عَلَيْهِ فَطَعَنَهُ رَسُولُ اللَّهِ –صلى الله عليه وسلم بِعُرْجُونٍ كَانَ مَعَهُ فَجُرِحَ الرَّجُلُ فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ –صلى الله عليه وسلم:« تَعَالَ فَاسْتَقِدْ ». فَقَالَ: بَلْ عَفَوْتُ يَا رَسُولَ اللَّه(من كتاب السنن الكبرى للبيهقي)
Na imepokewa na Abu Sa’id Al-Khudriy amesema: ”Wakati Mtume anagawa kitu fulani ghafla akatokea mtu na kumwangukia, akmchoma Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) yule mtu na mti aliokuwa ameushika na kumjeruhi, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) akamwambia yule mtu njoo ulipize kisasi, akasema: '‘Bali nimesamehe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu).
(As-Sunanu Al-Kubraa ya Imaam Al Bayhaqiy).
12. Sera Ya Kukataza Matumizi Ya Nguvu (Jihadi) Katika Kufikia Malengo Ya Kisiasa
Uislam haujakataza moja kwa moja kutumia nguvu katika kudai haki hasa kama mtawala anafanya dhulma za wazi na Waislamu wakiwa wamejianda kwa nguvu za silaha.
قال تعالى:﴿ وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ وَمِنْ رِبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ﴾(الأنفال:٦٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Waandalieni hao (makafiri) kila mnachokiweza katika nguvu na na ngome ya farasi ili muwatishe maadui wa Allaah na maadui wenu”
(Surat Al-Anfaal: 60).
وقال تعالى:﴿ إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آَمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنْفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أُولَئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ ﴾(الحجرات:١٥).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hakika Waumini wa kweli ni wale ambao wamemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kisha hawakuingiwa na mashaka na wakapigana kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hao ndio waumini wa kweli kabisa”
(Surat Al-Hujuraat: 15).
وقال تعالى:﴿ أَمْ حَسِبْتُمْ أَنْ تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنْكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ ﴾(آل عمران:١٤٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hivi mnadhani kuwa mtaingia peponi kabla ya (kujaribiwa) na Allaah na kujua ni wapi kati yenu wenye kuipigania Dini ya Allaah na ni wapi wenye Subira”
(Surat Al-‘Imraan: 142).
وقال تعالى:﴿ وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّهِ﴾(البقرة:١٩٣).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na wapigeni vita hao (makafiri) mpaka kusiwe na fitna na iwe Dini ni ya Allaah (inayofuatwa)”
(Surat Al-Baqarah: 193).
Ulimwengu umekiri matumizi ya nguvu katika nchi zifuatazo baada ya raia kudhulumiwa haki zao :
-Zanzibar katika mapinduzi ya mwaka 1964
-Msumbiji na Frelimo
-Kenya na Mau Mau
-Biafra Nigeria na Rais Nyerere alishabikia mtengano kwa sababu wakristo walikuwa wakidhulumiwa na Waislamu na aliandika kitabu 1966 (rejea gazeti la Majira la tarehe 16/11/2011 Uk.3) akidai kwamba umoja wa Kitaifa hauna maana endapo baadhi ya raia wanadhulumiwa.
13. Sera Ya Kukanusha Itikadi Ya Al-Walaa Wal-Baraa
Katika Uislam kutobaguana kwa msingi wa kidini ni kinyume cha Itikadi muhimu ya Al-Walaa wal-Baraa (kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allaah).
Udugu unaokubalika katika Uislam ni wa Imani tu.
﴿إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ﴾(الحجرات:١٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Hakika waumini (tu) ndio ndugu”
(Al-Hujuraat:10).
Kafiri sio ndugu wala rafiki wa waumini.
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
﴿قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآَءُ مِنْكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّى تُؤْمِنُوا بِاللَّهِ وَحْدَهُ﴾(الممتحنة:٤).
“Hakika kuna mfano mzuri kwenu kwa Ibraahiym na walio pamoja nae waliopowaambia watu wao, sisi tuko mbali na nyinyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah tumewakanusha nyinyi na umedhihiri uadui na bughdha baina yetu sisi na baina yenu milele mpaka mumuamini Allaah Peke yake.’’
(Al-Mumtahinah: 4)
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِمْ بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُمْ مِنَ الْحَقِّ﴾(الممتحنة:١)
Na amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Enyi Mlioamini msiwafanye adui yangu na adui wenu kuwa ni marafiki (wasaidizi) mna waangushia mapenzi na kwa hakika wamekufuru yale yaliowajieni katika haki”
(Al-Mumtahinah: 1)
Ama kubaguana kwa misingi ya Utaifa, Ukabila, Urangi, Uzawa, Uzalendo na msingi wa Kilugha ni jambo lililokatazwa katika Uislam.
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ﴾(الحجرات:١٣)
“Enyi watu hakika sisi tumewaumbeni kutokana na mwanamme mmoja na mwanamke mmoja na tukawajaalia kuwa mataifa mbali mbali na makabila mbali mbali ili mjuane, hakika mbora wenu mbele ya Allaah ni Mcha Mungu wenu zaidi.”
(Al-Hujuraat: 13).
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alikemea sana ugomvi baina ya Muhajirina (waliohama toka Makkah) na Answaar (wazawa wa Madiynah) kwa misingi ya Uzawa na Akasema:
“Enyi Waislam (mnagombana) kwa wito wa msingi wa Kijahiliya (Kikafiri) na mimi niko pamoja nanyi baada ya Allaah kuwaongoza katika Uislam? Uacheni kwani huo ni uvundo”
SURA YA SITA
Tafsiri Sahihi Ya Baadhi Ya Maneno Na Vifungu Vya Katiba Ya Jamhuri
1. Neno Ibada: Kwa Mtazamo Wa Uislam Ni Pana Sana
Wanachuoni wetu wanakubaliana kwamba ibada ni:
"كل ما يحب الله ويرضاه من الأقوال والأعمال الظاهرة والباطنة”
“Ni kila anachokipenda Mwenyezi Mungu na kukiridhia katika maneno na matendo ya dhahiri na ya siri (moyoni)”.
Malengo ya Kuumbwa kwetu:
قال تعالى:﴿ وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ﴾(الذريات:٥٦).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Sikuumba majini na watu isipokuwa kwa ajili ya kuniabudu Mimi tu”
(Adh-Dhaariyaat: 56).
Kumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hakuna maana ya kuswali, kufunga, kuhiji tu. Bali ndoa, kazi, biashara kuhukumiana kwa shari’ah ni ibada.
قال تعالى:﴿ قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴾(الأنعام:١٦٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hakika Swalah yangu na Ibada yangu (kuchinja) na uhai wangu na kifo changu ni kwa ajili ya Allaah Mola wa viumbe wote)”
(Surat Al-An’aam: 162).
Kuhukumu kwa haki ni Ibada.
قال تعالى:﴿ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ﴾(يوسف:٤٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hukumu ni miliki ya Allaah Ameamrisha musiabudu (chochote) isipokuwa Yeye tu)”
(Surat Yuusuf: 40).
قال شمس الأئمة السرخسى:إعلم أن القضاء بالحق من أقوى الفرائض بعد الإيمان بالله تعالى وهو من أشرف العبادات(المبسوط:١٦٥ ص٥٩،٦٠).
Amesema Shamsu Al-Aimmah As-Sarkhasi:
“Elewa kwamba kuhukumu kwa haki ni miongoni mwa faradhi kubwa baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu na hiyo ndio Ibada tukufu”
(Al-Mabsuutw, uk. 59-60).
2. Neno Halali Ni Hukmu Ya Kishari’ah Ni Kila Aliloliridhia Mola Kufanywa Kwa Mujibu Wa Shari’ah
Kwa mujibu wa katiba ukiuza pombe maadam unalipa leseni, kodi na pombe si ya magendo basi kazi hii ni Halali.
Kufanya muamala wa riba ni halali.
Kamari ni halali.
قال تعالى:﴿ إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنْصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ﴾(المائدة:٩٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hakika pombe na kamari na mizimu ni uchafu utokanao na matendo ya Shaytwaan jiepusheni nayo”
(Surat Al-Maaidah: 90).
وقال تعالى:﴿ وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا ﴾(البقرة:٢٧٥).
Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na Amehalalisha Mwenyezi Mungu biashara na ameharamisha riba”
(Surat Al-Baqarah: 275).
3. Neno Haki Ya Kuishi
Mtu akiua hauawi kwa sababu eti ana haki ya kuishi.
Katika kesi ya Attorney (Mwendesha mashtaka wa serikali) V/s Mbushumi (Kesi ya jinai Na.14, Dodoma 1991.) Katika kesi hii mtuhumiwa Mbushumi Mnywaga alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji ambapo kwa mujibu wa sheria, adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa.
Mshtakiwa (mtuhumiwa) katika kesi hii alidai mahakamani haki ya msingi ya kuishi kwa mujibu wa katiba.
Mahakama ilkubaliana nae na hivyo kumhukumu mshitakiwa kwenda jela maisha badala ya kunyongwa hadi kufa.
(Angalia kitabu, Haki na wajibu wa raia uk.23 kilichotolewa na C.P.T (Christian Prof.of Tanzania).
Katika Uislamu mtu anaeua kwa dhulma nae anauliwa kutekeleza kisasi.
قال تعالى:﴿ وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ﴾(البقرة:١٧٩).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Na mna (nyinyi) kwenye kisasi uhai enyi wenye akili”
(Surat Al-Baqarah: 179).
4. Haki Ya Usawa Kwa Wote
Katika Uislamu binaadam wote ni sawa katika asili, Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ﴾(الحجرات:١٣)
”Enyi wtu hakika Sisi Tumewaumbeni kutokana na mwanamme mmoja (Aadam) na mwanamke mmoja (Hawwaa) na Tukawajaalia kuwa mataifa mbali mbali na makabila ili mpate kujuana, hakika mbora wenu mbele ya Allaah ni Mcha Mungu zaidi kwenu”
(Surat Al-Hujuraat: 13).
Lakini hii haina maana kwamba mwanamme na mwanamke wamepewa haki na majukumu sawa kwa kila kitu.
Katika tangazo la haki za binaadam:
Kifungu 16(1) la mwaka 1948:
“Mwanamme na mwanamke pindipo wakifikia umri wa baleghe watakuwa na haki ya kuoana na kuasisi familia bila kikwazo kwa sababu ya nasaba, utaifa au dini, kwani wao wote wana haki sawa katika ndoa na wakati wa kusimamisha maisha ya ndoa na wakati wa mtengano’’ (uk.74).
(أنظر كتاب حقوق الإنسان في الإسلام للدكتور سليمان بن عبدالرحمن الحقيل(ط الثانية ١٤١٥ﻫ١٩٩٤ﻡ)
Tazama kitabu cha HAKI ZA BINADAMU KATIKA UISLAMU cha Dr. Suleiman Ibn Abdulrahmani Al Huqail chapa ya pili 1415H, 1994.
Tanzania ilitia saini mkataba wa kimataifa wa haki za binaadam 1966 na ukatiwa katika katiba mwaka 1966 ibara ya 9(f) nayo inasema hivi:
“Kwamba heshima ya binaadam inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata kanuni za tangazo la dunia kuhusu haki za binaadam”.
قال تعالى:﴿ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ اللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ لَا هُنَّ حِلٌّ لَهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ وَآَتُوهُمْ مَا أَنْفَقُوا وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَنْ تَنْكِحُوهُنَّ إِذَا آَتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ﴾(الممتحنة:١٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Enyi ambao mulioamini watakapowajieni wanawake Waumini wenye kuhama basi wapeni mtihani Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi kuhusu kuamini kwao, kama mkijua kwamba wao ni Waumini basi musiwarejeshe kwa makafiri, hao (wanawake) sio halali kwao wala wao sio halali kwao (kwa vile ni makafiri, na wapeni walichotoa (mahari), na wala si vibaya kwenu kuwaoa wao kama mtawapa mahari zao wala musiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu”
(Al-Mumtahinah: 10).
Kifungu hiki cha katiba kimempa mwanamke usawa wa mia kwa mia na mwanamme, katika Mirathi na Uongozi.
قال تعالى:﴿ فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنْثَيَيْنِ﴾(النساء:١٧٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Basi mwanamme ana mara mbili ya fungu la mwanamke”. (Surat An-Nisaa: 172).
وقال تعالى:﴿ الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَى بَعْضٍ﴾(النساء:٣٤).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Wanaume ni wasimamizi (viongozi) wa wanawake ni katika yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewaboresha baadhi yenu kwa baadhi.”
(Surat An-Nisaa: 34).
Waislam hawawezi kuwa sawa na watu waovu:
وقال تعالى:﴿ أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ﴾(القلم:٣٥).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Hivi tunawafanya Waislamu ni kama waovu!”
(Surat Al-Qalam: 35).
وقال صلى الله عليه وسلم:(لن يفلح قوم ولو أمرهم امرأة)رواه البخاري.
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam): “Hawatofaulu kamwe watu waliomfanya mwanamke kutawalia jambo lao”.
(Ameipokea Imaam Al-Bukhaariy).
Katika tangazo la Haki na Usawa la umoja wa mataifa kafiri anaweza kuwa sawa na muislam, hivyo kafiri anaweza kuoa binti wa Kiislam, katika Uislam jambo hilo halikubaliwi.
قال تعالى:﴿ وَلَا تُنْكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّى يُؤْمِنُوا ﴾(البقرة:٢٢١).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Wala musiwaoze washirikina mpaka waamini”. (Surat al Baqarah:221).
وقال تعالى:﴿ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ﴾(الممتحنة:١٠).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na wala msiwaweke wanawake wa kikafiri katika kifungo cha ndoa zenu”
(Surat Al-Mumtahinah: 10).
5. Haki Ya Kumiliki
Pamoja na kwamba Uislamu unampa mtu haki ya kumiliki na kutasarafu na mali aliyoichuma,
قال تعالى:﴿ لِلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِمَّا اكْتَسَبُوا وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِمَّا اكْتَسَبْنَ﴾(النساء:٣٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Wana wanaume fungu katika vile walivyovichuma na wanawake wana fungu katika vile walivyochuma”
(Surat An-Nisaa: 32).
Lakini, mtu hawezi kumuandikia mrithi wasia na huyo ambaye ameandikiwa wasia haruhusiwi kupewa zawadi ya 1/3 ya mali ya mtu.
قال صلى الله عليه وسلم:(إن الله قد أعطى كل ذي حق حقه فلا وصية للوارث)(رواه أبي داود وابن ماجه).
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam): ”Hakika Allaah Amempa kila mwenye haki haki yake, hakuna usia kwa mrithi)”
(Wameipokea Abu Daawuud na Ibn Maajah).
وقال صلى الله عليه وسلم:(الثلث،والثلث كثير(رواه البخاري ومسلم).
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam) juu ya kiwango anachostahiki kuandikiwa wasia :
“Theluthi, na theluti pia ni nyingi”
)Wameipokea Imaam Al-Bukhaariy na Muslim).
Sheria za nchi ni kinyume cha hayo kwa madai ya kutetea haki za kikatiba.
Katika kesi ya rufaa Na.5/1997 iliyosikilizwa na mahakama ya rufaa Dsm, kati ya Anwar Z. Mohamed vs Saidi Selemani Masuka, katika hukumu yake June 10, 1997, Jaji Ramadhani alihoji hukumu ya Jaji Msumi ya sept, 5, 1996, aliyetengua wasia unaodaiwa kuachwa na Rukia Ahmed kwamba mume wake Anwar Z. Mohamed arithi mali yake yote.
Katika hukumu yake Jaji Msumi wa mahakama kuu wakati huo alitoa hoja kwmba kwa mujibu wa shari’ah za Kiislam hakuna wasia kwa mrithi na hakuna wasia zaidi ya 1/3 ya mali.
Uamuzi huo wa Jaji Msumi ulipingwa na Jaji Korosso (wakili katika kesi hii) akiitaka mahakama ipuuze na itupilie kwa mbali shari’ah hiyo ya Kiislam kwa madai kwamba inavunja haki ya kikatiba kifungu cha 24 kinachompa mtu haki ya kumiliki na kutumia atakavyo. Hata hivyo Jaji Msumi alisisitiza kwamba Shari’ah na mirathi za Kiislam ni sehemu katika Qur-aan na ni lazima Waislam warithiane kwa Shari’ah hii. Na akaonya kuichezea Shari’ah hiyo ni sawa na kuichezea Qur-aan, jambo ambalo alisema Jaji Msumi hadhani kwamba yupo mtu mwenye kutakia mema nchi hii anaweza kulikaribia.
Jaji Ramadhani kwa upande wake alidai kwamba Jaji Msumi amejichanganya mwenyewe katika hukumu yake kwamba amezingatia “Udini” na uzalendo badala ya sheria. Na alisisitiza kanuni ya kutotambua sheria au kanuni zinazokiuka haki za kikatiba.
Waliotengua hukumu hiyo ni waheshimiwa majaji wa mahakama ya rufaa:
L. M. Makanja, D. Z. Lubavu na B. A. Samatta.
Katika kesi hiyo ya Anwar dhidi ya Saidi aliyekuwa mume wa marehemu Rukia Ahmed mwanamke aliyeolewa na Bw.Saidi. Marehemu aliandika wasia wa mali yake yote kwa mumewe Bw.Saidi akimwacha mwanawe wa kuzaa ndugu Anwar bila ya urithi wowote. Ndugu Anwar alikuwa mtoto wa marehemu lakini kwa mume mwingine. Mtoto wa marehemu alipinga kutambuliwa kwa wasia huo kwani ni kinyume cha Shari’ah za Kiislam na akakoseshwa kurithi.
(Angalia Sheria za Kiislam ya Mirathi na wasia) cha Mahmud A.Sameya uk.91 na 92).
6. Kufuta Adhabu Ya Viboko Ni Kinyume Cha Shari’ah Ya Kiislam
Kifungu 13(6) (e) Kinasema:
Ni marufuku kwa mtu kuteswa kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtesa au kumdhalilisha.
Uislam unaruhusu adhabu ya viboko.
قال تعالى:﴿ الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا مِئَةَ جَلْدَةٍ﴾(النور:٢).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanaume wapigeni kila mmoja mijeledi mia moja”
(Surat An-Nuur: 2).
وقال تعالى:﴿ وَالَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَأْتُوا بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ فَاجْلِدُوهُمْ ثَمَانِينَ جَلْدَةً﴾(النور:٤).
Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
”Na wale ambao wanawasingizia machafu wanawake wenye kujihifadhi na (machafu) kisha hawakuleta mashahidi wanne wapigeni mijeledi thamanini”
(Surat An-Nuur: 4).
وقال صلى الله عليه وسلم:(مروا أولادكم الصلاة وهم أبناء سبع واضربوهم عليها إذا بلغوا عشرة)(رواه أبوداود).
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa wa sallam):
”Waamrisheni watoto wenu Swalah wakiwa na umri wa miaka saba na wapigeni kwa kuacha Swalah watakapofika umri wa miaka kumi”
(Imepokewa na Abu Daawuud).
HITIMISHO
Wakati tukiwa katika hatua za mwisho za uandishi wa kitabu hiki, wananchi wote tumeshtukiziwa na Mswaada wa Sheria ya mwaka 2011 ambayo umekusudia kuweka masharti ya uanzishaji wa Tume, pamoja na sekretarieti kwa madhumuni ya kuendesha na kusimamia mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Cha kushangaza serikali ilitoa hati ya dharura kwa maana ya kwamba wananchi wachangie maoni juu ya Mswaada huu haraka haraka ili upitishwe na bunge kwa njia ya haraka. Muda uliotolewa ni mfupi mno na vituo vya kutoa maoni, vilipangwa kuwa ni vitatu tu Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar.
Wananchi wengi hawakuridhishwa na mchakato huu, jambo ambalo limepelekea zoezi hili kuakhirishwa ili wananchi wapewe muda zaidi wa kutoa maoni.
Baada ya kufaulu kupata nakala ya Mswaada huu tumegundua Mswaada huu una mapungufu mengi lakini makubwa katika hayo ni lile la kuwafunga wananchi wasiyaguse yale ambayo kwa mtazamo wa waliotunga Mswaada huu ni tunu na maadili matakatifu ya kitaifa hivyo yasipingwe katika hayo ni yale yaliyokuja katika kipengele cha 9 (2) :
(a) Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
(b) Msingi /Asili ya Usekula (kutenganisha siasa na dini) ya Jamhuri ya Muungano.
Masharti haya hayakubaliki kwa sababu yanawanyima raia ambao ndio watunzi halisi wa katiba, Uhuru wa Maoni ambao wamepewa na kipengele cha 18 (1) na 19 (1) cha Katiba ya nchi hii.
Upande wetu Waislamu wazo la kuifanya nchi hii idumu kuwa ni ya kisekula inayotenganisha Dini na Utawala ni wazo lisilokubalika hasa ukizingatia kwamba wazo lenyewe asili yake ni Dini ya Kikristo kama tulivyoona katika kitabu hiki. Wazanzibari kwa mfano ambao wana nchi yao yenye wakazi asilimia 99 Waislam wana haki ya kutangaza kwamba nchi yao ni ya Kiislamu yenye kufuata Shari’ah za Kiislam, wenyewe wana haki ya kufanya maamuzi haya.
Kitabu hiki tunataraji kitakua ni msaada mkubwa wa Rejea kwa kila anaetaka kuchangia maoni ya Utunzi wa Katiba mpya, kwa sababu kimetoa picha ya Makosa ya Msingi yaliyomo ndani ya Katiba iliyopo. Hivyo marekebisho yoyote ni lazima yachunge mtazamo huo.
Mola Atupe Tawfiq.
18/5/1432 H sawa na 22/4/2011 M